Siri nzito Majizzo na Mbowe kupeana maua mtandaoni


Hivi karibuni umeibuka msemo wa nipe maua yangu kabla sijafa msemo uliochagizwa na wimbo wa mwanahiphop Roma Mkatoliki aliye ughaibuni.

Udhihirisho wa msemo huo umeonekana kwa mfanyabiashara Francis Ciza maarufu kwa jina Majizzo kupitia mtandao wa twita ambapo alimshukuru Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.


Majizzo aliandika “Freeman Mbowe Kwangu ni Legend upande wa burudani. Naonaga wakimuita ‘DJ’ kama utani, but me being a DJ huo ‘uDJ’ ndio nyota. Hakuwa DJ lakini aliajiri DJs”

Kwenye biashara zangu za Club, tulijifunza na kuiga mengi Bilcanass, nina heshima kubwa kwa Mbowe na familia yao.



Baada ya tweet hiyo Mbowe naye hakusita kumjibu na kumwambia “Maisha ni kujitafuta, hili ni somo kubwa ambalo kila mtu hasa vijana wanatakiwa kulitilia maanani”


Ujumbe muhimu wa Mbowe kwa Majizzo ukawa “Ni lazima utafute nafasi ya kufanikiwa hadi ujipate.  Safari, mapambano na hatua unazopiga  Majizzo ni hamasa kubwa kwa vijana kutafuta bila kuchoka, hongera sana na kila la kheri”

Majibizano ya kupeana maua yameendea ambao Majizzo hakusita kumjibu tena Mbowe kwa kuandika “Moyoni nimefarijika sana kuamka na kukutana na ujumbe wa bro Mbowe. Again, thank you Freeman Mbowe. Sisi tutaendelea na harakati za biashara na huduma hii mliyoifanya vizuri sana pale Bilcanass tukajifunza.” 

TAFSIRI YA LEGENDKumekuwepo na mvutano wa watu maarufu kuitana malegend ikiwa na maana ya nguli walionesha weledi mkubwa katika fani zao.


Wakati mmoja huko mtandaoni msanii Rashid maarufu Chidbenz alionekana kubishana na mwandishi wa habari wakati wa mahojiano akiwa na Joseph Haule maarufu Professa Jay 

Mabishano kati ya mwandishi na Chidbenz yalitokana na yeye kulinganishwa na Prof Jay katika kauli ya Chid alisema “Huwezi niita mimi legend mbele ya Prof Jay ambaye nilikuwa nikimtamzama toka nikiwa shuleni huyu ni legend mimi niite Muki” 

Jambo hilo lilitafsiriwa na kufikirisha zaidi kuwa wapo wasanii wachache na chipukizi ambao wanaweza kuonesha nafasi za watangulizi wao katika tasnia.



Chapisha Maoni

0 Maoni