Wizara ya Maji yaomba bilion 756.2 mwaka 2023/24

Waziri wa Maji  Jumaa Aweso ameliomba  bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi 756,205,106,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2023/24. 

Akiwasilisha mapendekezo hayo bungeni Aweso amesema Kati ya fedha hizo, matumizi  ya Kawaida ni Shilingi 60,375,474,000 ambapo Shilingi 18,035,561,000 sawa na asilimia 29.87 ni kwa ajili ya kugharamia Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 42,339,913,000 sawa na asilimia 70.13 ni kwa ajili ya kulipa Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara, RUWASA na Chuo cha Maji. 

Amesema jumla  ya bajeti ya maendeleo ni Shilingi 695,829,632,000 ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 407,064,860,000 sawa na asilimia 58.50 ni fedha za ndani na Shilingi 288,764,772,000 sawa na asilimia 41.50 ni fedha za nje.

Hali ya maji 

Aweso amesema takwimu zinaonesha kuwa mahitaji ya maji nchini kwa sekta mbalimbali mwaka 2022 yalikuwa ni wastani wa mita za ujazo bilioni 62 na yanatarajiwa kuongezeka na kufikia mita za ujazo bilioni 80.2 mwaka 2035. 


Mahitaji hayo yataendelea kuongezeka kutokana na ongezeko la watu, ukuaji wa shughuli za uzalishaji mali katika sekta mbalimbali hususan kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa umeme, uzalishaji viwandani, utalii, uchimbaji madini, ufugaji, uvuvi na wanyama pori. 


Kwa upande mwingine, uharibifu wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji, uhaba wa mvua unaotokana na mabadiliko ya tabianchi na matumizi mabaya ya maji husababisha kupungua au kukauka kwa maji katika vyanzo.

18.

Mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara ya Maji iliidhinishiwa 709,361,607,000 na kati ya fedha hizo Shilingi 51,462,269,000 zilikuwa ni fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi 657,899,338,000 zilikuwa ni fedha za maendeleo. 


Hadi mwezi Aprili 2023, Wizara hiyo imepokea jumla ya Shilingi 686,370,565,613.50 sawa na asilimia 96.76 ya bajeti iliyoidhinishwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni