Trump atiwa hatiani kwa kumdhalilisha kijinsia mwandishi

 


Mahakama imemtia hatiani aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump kwa kumdhalilisha kijinsia mwandishi wa makala kwenye jengo moja New York katika miaka ya 1990.

Hata hivyo mahakama haijamtia hatiani Trump kwa kumbaka mwandishi huyo E Jean Carroll katika chumba cha kubadilishia nguo cha Bergdorf Goodman.

Mahakama pia imemtia hatiani Trump kwa kukashifu kutokana na kumtuhumu mwandishi huyo kuwa “tapeli na muongo”.

Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutiwa hatiani kisheria na mahakama kuhusiana na tuhuma za udhalilishaji kijinsi zinazomuandama.




Chapisha Maoni

0 Maoni