Waziri Ummy afafanua watu sita kukutwa na corona

 

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona wiki ya kuanzia May 6 - 12, 2023, ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya April 29 hadi May 05,2023, hakuna kifo chochote kilichothibitishwa kusababishwa na Covid-19.


 Waziri Ummy ameyasema hayo kupitia mtandao wa twita wakati akifafanua kuhusu tetesi za uwepo wa mlipuko mpya wa Covid 19 Tanzania.

Ummy amewaomba Wananchi waondoe hofu na kusema Wizara ya Afya inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali au Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii kisha watatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au lah!



“Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili, nawaomba Wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi” ameandika 

Chapisha Maoni

0 Maoni