Waziri Mkuu Finland kuondoka madarakani na kwenye ndoa

 


Waziri Mkuu wa Finland anayeondoka madarakani Sanna Marin na mumewe Markus Raikkonen wamewasilisha nyaraka za kutalikiana.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Bi. Marin ameandika “Tulikuwa na maisha ya faraja ya pamoja kwa miaka 19 pamoja na binti yetu mpendwa”.

Wanandoa hao walifunga ndoa 2020, wakati Bi. Marin alipokuwa akiliongoza taifa la Finland kipindi cha mlipuko wa Covid-15, na wamejaliwa binti wa miaka 5.

Waziri Mkuu Marin anatarajia kuondoka madarakani baada ya chama chake chenye kufuata siasa za mrengo wa kati wa kushoto kushindwa katika uchaguzi mkuu mwezi uliopita.

Katika posti yake kwenye Instagram, Bi. Marin amesema mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwanasoka wa zamani bado ni rafiki yake bora.

Chapisha Maoni

0 Maoni