Ajabu watoto waelea siku tatu ziwani DRC bila kufa

 


Watoto wawili wachanga wameokolewa wakiwa wanaelea kwenye ziwa Kivu, siku kadhaa baada ya kutokea mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 400 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Mmoja wa viongozi wa serikali ya mtaa Delphin Birimbi amesema kwamba “Ni muujiza kupatikana kwa watoto hao wakielea majini, kila mtu anastajabu”.

Birimbi amesema wazazi wa watoto hao wamekufa kwa mafuriko, lakini jamii imewasiliana na watu ambao wapo tayari kuwalea.

Haijajulikana ni kwa jinsi gani watoto hao wameweza kuishi siku tatu majini wakielea kwenye takataka zilisosomwa na maji.

Chapisha Maoni

0 Maoni