Watu wanane wauawa kwa risasi dukani Marekani


Mtu mwenye silaha amewafyatulia risasi na kuwaua watu wanane kwenye duka la bidhaa kaskazini mwa Dallas, watoa huduma wa dharura Texas wamesema.

Mamia ya watu wameondolewa kwenye jengo la duka la Allen Premium, ambapo mashuhuda wamesema mtu huyo alifyatua risasi hovyo kwa watu wapitao.

Afisa mmoja wa polisi aliyekuwapo katika eneo la tukio ameuawa kwa risasi na mtu huyo.

Baadhi ya wahanga wa tukio hilo ni watoto. Watu wapatao saba wanatibiwa hospitalini, watatu miongoni mwao hali zao ni mbaya.

Chapisha Maoni

0 Maoni