Bloga maarufu auawa kwa kupigwa risasi Uganda

 


Bloga maarufu nchini Uganda Ibrahim Tusubira aka Isma Olaxes ameuawa kwa kupigwa risasi katika kitongoji cha Kyanja.

Tusubira alifariki papo hapo baada ya gari lake lenye usajili namba UBK213D kushambuliwa kwa risasi usiku wa jumamosi nje ya geti la nyumba yake.

Taarifa ya polisi imesema kuwa Tusubira ameuawa wakati akiendeshwa na dereva wake aliyetambuliwa kwa jina la Wasswa Mathias.

Hivi kribuni Bloga Tusubira ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Mabloga Uganda alinukuliwa akisema kunawatu wanapanga kumuua.

Chapisha Maoni

0 Maoni