Watuhumiwa mauaji ya daktari Isack na mfanyakazi GGM wanaswa

 


Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema limefanikiwa kuwakamata watu watatu wanaotuhumiwa kumuua Dk Isack Daniel Athuman.


Taarifa  iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime imesema watuhumiwa hao watatu wamekamatwa mkoani Mwanza baada ya kufanya mauwaji ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Karende kilichopo Tarime Rorya wakati akitoka kazini.




Jeshi hilo limeeleza baada ya watuhumiwa kutenda kosa hilo walikimbilia Mwanza na kisha mkoani Dar es Salaam ambapo askari wa uchunguzi waliwabaini na kuwakamata.



 Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime  imebainisha pia kuwakamata watuhumiwa watatu waliohusika kumuua mfanyakazi wa GGM Milembe Seleman Hungwa April 26,2023 na uchunguzi zaidi unaendelea ili kuwafikisha mahakamani. 

SOMA ZAIDI


Chapisha Maoni

0 Maoni