Mtuhumiwa mauaji ya Milembe wa GGM ajinyonga

 

Mtuhumiwa  wa nne kati ya watatu waliokamatwa kwa tuhuma za mauwaji ya mfanyakazi wa GGM amejinyonga kwa mkanda wa suruali.


Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya mfanyakazi kitengo cha ugavi GGM Milembe Seleman yaliyotokea April 26, 2023.


SACP Misime amesema mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina Pastory Lugandisha baada ya kupata taarifa za kukamatwa wenzake na askari kufika nyumbani kwake, Mei 6, 2023 alijihukumu kwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali katika pori la hifadhi ya Buhindi Sengerema.



Marehemu Milembe alikutwa na majeraha ya kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani, usoni na mikononi ambapo kiganja kimoja cha mkono kiliondolewa.

Chapisha Maoni

0 Maoni