Sita wadakwa kwa kumuuzia mteja chupa badala ya madini ya copper

 

Watuhumiwa  6 kati 9 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa makosa ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji fedha haramu.


Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo May 11 katika  kesi Na 11/2023 mbele ya Mhe. Hakimu Urio mahakama hiyo.

Inadaiwa kuwa katika kipindi cha Sept 2022 washtakiwa kwa kutumia Kampuni ya Steca Export Co. Ltd, walifanya biashara ya kuuza Madini ya Copper yenye thamani ya sh. 1.6 Bilion kwa Kampuni ya Zhejiang Afol ya nchini China.

Kwamba washtakiwa walisafirisha chupa tupu za vinywaji (wine beverages bottled) badala ya Madini ya Copper, waliyomuuzia mlalamikaji kupitia Clearing Agent ya Mwikolo Logistic & Globvest Group Ltd. 


Imethibitika kwamba chupa tupu zilisafirishwa kwa makontena 5 kwenda China kupitia wakala wa meli MAERSK.


Uchunguzi unaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine 2 pamoja na mali zao.

Washtakiwa wamerudishwa  rumande katika gereza la Segerea kufuatia kutuhumiwa  na  makosa ambayo hayana dhamana.

Chapisha Maoni

0 Maoni