Rais Mwinyi avihakikishia ushirikiano vyombo vya habari na serikali asisitiza hakuna uhuru usio na mipaka


 Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema,  serikali  zote mbili zitaendelea  kushirikiana kwa karibu na vyombo vyote vya habari katika kutatua changamoto  zinazowakabili wanahabari .


Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Mei 3, 2023 Zanzibar katika maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ambapo amewataka wanahabari kuwa wazalendo kwa nchi , na kusisitiza hakuna uhuru usio na mipaka na  uhuru usio na wajibu.


Dk Mwinyi ametaka madhimidho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani yatumike kama fursa ya kuweka mkazo katika uhuru  wa kujieleza ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binadamu. 


Amesema usajili wa vyombo vipya vya habari nchini umeongezeka kwa kasi kubwa jambo lililofanya uhuru wa kujieleza na kusambaza  habari kuongezeka.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic amesema uhuru wa vyombo vya habari ni kichocheo cha kuimarisha haki nyingine.

“UN nchini Tanzania inatambua hitaji hili na itaendelea kushirikiana na serikali, washirika, na vyombo vya habari ili kuimarisha upatikanaji wa habari kwa manufaa ya umma,”


Zlatan  ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini ,licha ya kukosolewa vikali na baadhi ya Watanzania wanaodai kwamba uhuru huo unatumika kueneza ushoga na usagaji.

Chapisha Maoni

0 Maoni