Msako huo wenye lengo la kuyabaini makanisa yasiyosajiliwa na yanayotoa mafundisho utata umemkamata katika eneo la Bungoma.
Mhubiri huyo anajulikana kama Nabii Yohana kutoka Kenya, ametakiwa kufika mbele ya Kamanda wa Polisi wa Bungoma, Juni 2, mwaka huu kwa ajili ya kujieleza.
Mhubiri huyo mwenye umri wa miaka 83 anaendesha kanisa liitwalo Church for All Nations amekuwa na kishindo cha kustaajabisha haswa baada ya madai ya kuzindua biblia yake yenye vitabu 93 na sarafu yake.
Kwa mujibu wa Franci Kooli, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Bungoma, amesema mhubiri huyo atahojiwa na kuchunguzwa kwa madai ya mafundisho yenye utata na jinsi kanisa lake linavyofanya kazi.
Katika biblia yake inasemekana kuwa alibuni na kuongeza amri zake mwenyewe, akiongeza amri mbili zaidi katika zile kumi ambazo hujulikana katika dini ya Kikristo.
0 Maoni