Ndege ya Kanisa yakutwa na kilo 290 za bangi

 

Polisi wamekamata kilo 290 za bangi kwenye ndege iliyosajiliwa kwa jina la tawi la kanisa moja la Kiinjilisti la nchini Brazili.

Ndege hiyo yenye injini moja ilikuwa inajiandaa kuondoka kwenye hema la kuhifadhia ndege katika  uwanja wa kimataifa wa Belém.

Mtu mmoja amekamatwa katika eneo la tukio, licha ya kujaribu kutaka kukimbia vyombo vya dola.

Picha zilizotolewa na Polsi wa Shirikisho wa Brazili zinaonyesha bangi hiyo iliyobainika kwenye ndege hiyo ya kanisa.

Chapisha Maoni

0 Maoni