Manchester City imewachachafya vinara wa ligi kuu ya England Arsenal kwa kuichabanga magoli 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Etihad katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England.
Kwa sasa vinara hao wa ligi hiyo, wanakalia kuti kavu kileleni baada ya Manchester City kuwasogelea kwa tofauti ya alama mbili huku wakiwa wamecheza mechi mbili zaidi ya mabingwa hao watetezi.
Msimamo wa EPL kwa sasa uko hivi:-
ARSENAL—Mechi 33—Alama 75
MAN CITY—Mechi 31—Alama 72
Newcastle—Mechi 31—Alama 59
Man United—Mechi 30—Alama 59
Mchezaji Kevin De Bruyne amefunga magoli 8 dhidi ya Arsenal kwenye ligi kuu England ambapo jana alifunga magoli mawili kwenye dakika ya 6 na 53 ya mchezo wengine waliofunga ni Stone 45+1' Haaland dk 90+5 na Holding dk 86.Arsenal ya Mikel Arteta, ilishinda taji hilo mara ya mwisho mnamo 2003-04, chini ya kocha Arsene Wenger.Wakiwinda taji la tano la Premier League ndani ya miaka sita, City pia wako kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 Maoni