Mhe. Ndejembi, Guterres wazungumzia mageuzi ya UN na amani duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres, katika Makao Makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, tarehe 25 Septemba 2026, ambapo amempongeza kwa uongozi wake na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za mageuzi ndani ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Mhe. Guterres ameipongeza Tanzania kwa kuwa mshirika muhimu wa Umoja huo na kuthamini mchango wake katika amani na usalama duniani.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, yakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kuendeleza juhudi za mageuzi, amani, usalama na ushirikiano wa kimataifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni