Na. Kassim Nyaki- Ngorongoro
Mbio za Mwenge wa Uhuru jana tarehe 6
Julai, 2026 zilliwasili Wilaya ya Ngorongoro na kukimbizwa umbali wa
kilomita 386 kuzindua miradi mbalimbali ambapo pia umepita katika
eneo la hifadhi ya Ngorongoro na kuangazia maajabu saba ya Ngorongoro
huku watalii kutoka mataifa mbalimbali wakishuhudia.
Ukiwa
katika hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Wilaya ya Karatu watalii kutoka
mataifa mbalimbali walionyesha bashasha kuona Mwenge ukipita eneo la
hifadhi lenye vivutio mbalimbali ambapo tukio hilo linaashiria uwepo
wa Amani, umoja na mshikamano wa Kitaifa unaotoa tumaini kwa wageni
kufanya shughuli za utalii bila changamoto yoyote.
Mmoja wa
wageni kutoka nchini Denmark Ella Wiliams ameeleza kuwa “Tumefurahi
kuona Mwenge wa Uhuru ukipita eneo la hifadhi kwa hali ya utulivu na
sisi kuwa sehemu ya tukio hili, hii inaashiria kuwa Tanzania pamoja
na kuwa na maajabu mengi ya vivutio vya utalii, ni nchi pia yenye
amani, umoja na mshkamano unaoshiria Taifa moja lenye watu
wanaopendana na kushirikiana”
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru
Kitaifa Bw. Wazo Michael Mwang’onda ameeleza kuwa; Ngorongoro ni
hifadhi yenye vivutio vingi vya utalii na hadhi za kimataifa ambapo
yeye na timu ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wanahamasisha
amani,umoja na mshkamano wa kitaifa ili kwa pamoja kuletea maendeleo
kupitia fedha za kigeni zinazochangiwa na idadi kubwa ya watalii
wanaotembelea hifadhi za Ngorongoro na maeneo mengine ya
nchi.
Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
wakiongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia
Idara ya Wanyamapori na Utafiti Vicktoria Shayo, wameshiriki mbio
kupokea Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ngorongoro na kuukabidhi leo
tarehe 7 Julai, 2026 katika Wilaya ya Karatu.


0 Maoni