Katika Viwanja vya Sabasaba, timu ya Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro ikiongozwa na Kamishna wa Uhifadhi Abdul-Razaq
Badru tarehe 6 June, 2026 ilivifunika viwanja hivyo huku macho na
masikio ya wananchi waliotembelea yakijielekeza kwenye Kampeni ya
Ngorongoro inayojulikana kama Karibu Nyumbani.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari katika siku maalum ya Ngorongoro, Kamishna Badru
amewaeleza kuwa umuhimu wa kampeni hiyo inatokana na historia kwa
kuainisha wazi kuwa binadamu wa kale kutembea kwa miguu miwili
historia yake alipatikana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Ameeleza
kuwa ushahidi uliopo wa zaidi ya miaka milioni 3.6 unaonesha binadamu
huyo aliweza kutembea na kufanya shughuli zake kwa kutumia zana za
miaka hiyo, kuyatawala mazingira na kuishi bila shida
yoyote.
Mhifadhi Mambokale wa Ngorongoro Ladislaus Kashaija
akitoa maelezo kuhusu kwanini Ngorongoro inajivunia historia hiyo
ameeleza kuwa inatokana na ushahidi wa wanazuoni duniani kote kuitaja
Ngorongoro kama sehemu yenye ushahidi wa kutosha kuhusu historia ya
binadamu.
Mchezaji wa timu ya soka ya Simba Shomari Kapombe
amesema kuwa atakuwa chachu ya luwashawishi wanasoka wenzie
kuitangaza Ngorongoro kuwa chanzo cha mpira wa miguu kwa kuwa
historia ya binadamu kutembea kwa miguu miwili imeanzia
hapo.
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeshiriki tukio la
siku ya Ngorongoro (Ngorongoro Day) katika viwanja vya sabasaba kwa
kuhamasisha washiriki warudi Nyumbani Ngorongoro kwani mwenda kwao si
mtumwa.





0 Maoni