Jeshi la Polisi Nchini limesema hali ya usalama nchini ni shwari hadi kufikia mchana wa leo Julai 7, 2026 huku likiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudumisha amani na utulivu.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime, amesema licha ya leo kuwa siku ya mapumziko ya Sikukuu ya Sabasaba, wananchi wengi wameendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii katika mazingira ya utulivu.
Amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama litaendelea kuimarisha ulinzi nchini ili wananchi waendelee na shughuli zao kwa amani.
Pia amewataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kujiepusha na kusambaza taarifa za uongo, kuchochea chuki au kuvunja sheria, akisisitiza kuwa kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria.

0 Maoni