Na. Beda Msimbe (TBN)
Moscow
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia
Suluhu Hassan amesema wakati umefika kwa Tanzania na Urusi kutekeleza
makubaliano na kuacha maneno katika kufanikisha makubaliano
yanayokuza biashara na uwekezaji.
Amesema kwamba uwekezaji
Tanzania unalipa hasa katika mikakatik ambayo imelenga kutekeleza
Dira ya maendeleo ya 2050.
Alisema kwamba milango ya Tanzania
ipo wazi kuona kwamba makubaliano ya ujenzi wa viwanda vya dawa, viua
dud una uwekezaji kwimngine unfanyuiwa kazi kwa manjufaa ya pande
zote mbili.
Alisema ikiwa sehemu ya kurahisha utekelezaji wa
mikataba ya uwekezaji kuanzia Julai 2 mwaka huu Shirika la Ndege
(ATCL) litaanza safari za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam, Moscow
na Zanzibar.
Aidha ni matarajio ya Rais Samia kwamba Shirika
la Ndege la Urusi la Azur pia litanza safari hizo.
Akizungumza
na wafanyabiashara juu ya nafasi ya wananchi wa pande zote mbili
kunufaika na uhusiano huo, Rais Samia alizungumzia kuhusu uwekezaji
wa Urusi nchini Tanzania na kuwaita wafanyabuashara na wawekezaji
katika nishati, madini, dawa za binadamu, viwatilifu na kilimo na
kusema mabadiliko makubwa yanatakiwa kufanywa ili kupunguza urari wa
biashara.
Alisema kwamba ujazo wa sasa biashara hauakisi
ukweli kuwa kuna nafasi kubwa ya kuwapo kwa maendeleo ya ushirikiano
hasa katika n yajna ambazo ni za kimkakati zinazolenga kuihudumia
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Naye Waziri wa Maendeleo
ya Kiuchumi wa Urusi, Maxim Reshetnikov amesema kwamba amefurahishwa
na juhudi za kuifungua Tanzania zinazofanywa na Rais Samia Suluhu
Hassan.
Alisema juhudi hizo zinazaa matunda na kwamba Urusi
ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi yake ya
kimkakati.
Anasema taifa hilo litaendelea kufungua fursa
mbalimbali kwa kuwekeza nchini Tanzania katika kilimo na teknolojia
na viwanda
“Tanzania ni lango la mashariki ya kati tupo
tayari kuwapatia teknolojia na utaalamu wetu na tupo tayari kushiriki
katika kuanzisha viwanda mbalimbali vya dawa na mbolea” alisisitiza
waziri huyo akishukuru kwa namna ambavyo wafanyabiashara wa Tanzania
walivyofika kwa wingi baada ya mkutano wa Arusha, kushiriki katika
ukamilishaji wa mambo mbalimbali.
Aidha mmoja wa
wafanyabiashara wa Kitanzania akizungumza baada ya kukamilika kwa
kongamano hilo, Dhruv Jog, amesema kualikwa kwa wafanyabiashara
katika safari ya Rais na kushiriki kongamano hilo inaonesha ni kwa
namna gani sekta binafsi inathaminiwa katika kubadili maisha ya
Watanzania.
Alisema kitendo hicho kinasaidia kuifungua
jumuiya ya sekta binafsi katika daraja jingine. Alisema kufanikiwa
kufungua soko la Urusi kutawezesha watanzania kufanya biashara na
nchi takribani 15 zinazofanya ukanda wa Urusi hivyo kuleta kipato
zaidi.
Katika ziara hii ya kihistoria ikifanywa kwa mara ya
pili katika historia ya uhusiano wa Tanzania na Urusi, ya kwanza
ilikuwa ni miaka ya 1960 iliyofanywa na baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere, Rais Samia anaendeleza kampeni kubwa ya kuhakikisha Tanzania
inanufaika pia kiuchumi na uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali.
Akiwa hapa Rais Samia alifanya mazungumzo na Rais Vladmir Putin
katika lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kisiasa,
kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi
Pia Rais
Samia ameiweka Tanzania katika ramani ya uwekezaji kwa hotuba yake
aliyoitoa katika mkutano mkubwa wa uwekezaji jijini St Petersburg.



0 Maoni