Mchungaji Richard
Hananja amewataka vijana kutafakari kwa kina kabla ya kushiriki
katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi,
akisisitiza kuwa tofauti za mitazamo zinapaswa kuwa chachu ya
mazungumzo na maelewano badala ya kusababisha migawanyiko katika
jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,
Hananja amesema matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii
yanaweza kuchochea chuki, matusi na vurugu, hali inayoweza kuathiri
mshikamano wa kitaifa.
Amehimiza vijana kutumia majukwaa ya
kidijitali kwa uwajibikaji, kuheshimu maoni ya wengine na kuendeleza
maadili yanayojenga umoja, amani na maendeleo ya jamii.
Hananja
amesisitiza kuwa vijana wana nafasi muhimu katika kulinda amani ya
taifa na kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kijamii na kisiasa
unapaswa kuongozwa na busara, heshima na uzalendo.

0 Maoni