Tanzania imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini huku bei zake zikisalia kuwa nafuu zaidi ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani.
Bei mpya zilizotangazwa na EWURA kuanzia Juni 3, 2026 zinaonyesha kuwa petroli katika Dar es Salaam itauzwa kwa Sh. 4,086 kwa lita, dizeli Sh. 4,333 na mafuta ya taa Sh. 4,685 kwa lita.
Petroli imepungua kwa zaidi ya shilingi 30 kwa lita ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku dizeli ikiendelea kunufaika na ruzuku ya shilingi 535 kwa kila lita.
Licha ya changamoto zinazoikabili dunia kutokana na migogoro inayoendelea Mashariki ya Kati na athari zake katika biashara ya mafuta, Tanzania imeendelea kudhibiti ongezeko la bei na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini.
Ruzuku ya dizeli imeendelea kusaidia sekta muhimu za uchumi ikiwemo usafirishaji, viwanda na kilimo, hatua inayochangia kupunguza gharama za uzalishaji na huduma kwa wananchi.

0 Maoni