Maadhimisho ya siku ya Urithi wa Dunia Afrika yaliyofanyika katika Makumbusho ya Urithi Jiopaki mjini Karatu tarehe 5 Mei, 2026 yameyakutanisha makabila makuu manne yanayounda Jiopaki ya Ngorongoro Lengai ambayo ni wamasai, wahadzabe, wairaqw na wadatoga na hivyo kuunganisha kutaniko kubwa la urithi wa dunia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkuu wa wilaya ya Karatu
Mhe. Dkt Lameck Karanga amesema uwepo wa makabila hayo, historia yao
pamoja na kuenzi tamaduni zao ni utajiri mkubwa kwa Tanzania na kutoa
wito kwa wadau na jamii kwa ujumla kuendelea kulinda maeneo ya urithi
wa dunia na kuibua maeneo mapya yatakayoingizwa katika orodha ya
Urithi wa Dunia ili kuongeza thamani ya ubora wa kipekee ulimwenguni
(Outstanding Universal Value) na kuvutia wageni wengi zaidi.
Naibu
Kamishna wa Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii Ngorongoro Joas
Makwati ameeleza kuwa mamlaka itaendelea kuongeza juhudi za
kulihifadhi eneo la Ngorongoro ambalo ni urithi wa dunia na
kultangazia zaidi kama eneo pekee lenye Ushahidi wa kisayansi kuhusu
historia ya binadamu unaoeleza kuwa binadamu kwa kuthibitishwa na
ugunduzi wa masalia ya binadamu wa kale na zana za mawe
zilizopatikana katika bonde la Olduvai.
Kwa upande wake Naibu
Katibu wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania Dkt. Khamis Said ameeleza
kuwa tangu Tanzania ijiunge na UNESCO imepata mafanikio mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuridhia mikataba kumi (10) ya UNESCO,Kuwepo kwa
Hifadhi Hai za Mwanadamu na Mazingira sita (6) na Kuwepo kwa maeneo
saba (7) ya urithi wa Dunia.
Kauli mbiu ya siku ya urithi wa
dunia kwa mwaka huu ni “Kusherekea siku ya Urithi wa Dunia na
kukuza Viongozi wa baadaye”. (Celebrating Africa’s Heritage,
Mentoring the Leaders of Tomorrow).


0 Maoni