Mchambuzi
wa masuala ya uongozi, uchumi na siasa nchini, Dkt. Netho Ndilito
amesema ripoti ya Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani
wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imeleta mwanga
mpya kuhusu hali halisi ya taifa na changamoto zilizokuwa
zikijadiliwa kwa muda mrefu.
Amesema baada ya kupitia maoni ya
Watanzania, wanamitandao na wachambuzi mbalimbali, ameona ripoti hiyo
ni nyaraka muhimu iliyofichua mambo makubwa yenye maslahi kwa
taifa.
Kwa mujibu wake, ripoti hiyo imeliponya taifa kwa
kuweka wazi ukweli ambao kwa muda mrefu haukupata nafasi ya
kujadiliwa hadharani, ikiwemo kufichua nia na dhamira za baadhi ya
watu waliotamani vurugu kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Aidha,
ameeleza kuwa ripoti hiyo imeweka bayana upotoshaji na taarifa zisizo
sahihi zilizokuwa zikisambazwa na baadhi ya watu wasiolitakia mema
taifa, huku wakitamani kuona nchi ikiingia kwenye machafuko.
Pia
amesema ripoti hiyo imeonesha namna Watanzania wengi wanavyoipenda
nchi yao, kuiamini serikali yao na kutokuwa tayari kushawishika
kuivuruga amani, umoja na mshikamano wa taifa.
Vilevile,
imebainisha uimara wa serikali pamoja na ukomavu wa vyombo vya ulinzi
na usalama katika kushughulikia masuala ya ndani kwa weledi na
utulivu.
Dkt. Ndilito amewapongeza Watanzania kwa kuendelea
kudumisha umoja, upendo, mshikamano na amani, akisisitiza kuwa huo
ndiyo msingi wa heshima ya taifa kwa muda mrefu.

0 Maoni