Chama cha Wananchi CUF chahimiza maridhiano

 

CHAMA cha Wananchi CUF kimetoa msimamo wake kuhusu ripoti ya Jaji Othman Chande iliyohusu matukio ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kikitaka serikali kujikita zaidi katika maridhiano ya kweli na mchakato wa uponyaji wa taifa.

Chama hicho kimesisitiza umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa vurugu, ikiwemo kuwapatia matibabu ya kimwili na kisaikolojia pamoja na msaada wa kijamii.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu achaguliwe kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mwenyekiti wa CUF Taifa, Mirambo Kamili Yusufu, alisema chama hicho hakioni ulazima wa kujadili kwa kina ripoti hiyo kwa kuwa ni ripoti ya Rais iliyotengenezwa kitaalamu kwa lengo la kudumisha amani ya nchi.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa maridhiano ya kweli na uponyaji wa taifa ni mambo ya msingi, sambamba na hitaji la kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba mpya.

Aidha, Yusufu alizungumzia hali ya kisiasa na kiusalama Mashariki ya Kati, akieleza kuwa migogoro inayoendelea, ikiwemo vita vinavyohusisha Iran, Marekani na Israel, ina athari za kiuchumi duniani.


Alisema kuwa endapo chama hicho kingekuwa madarakani, kingeimarisha mfuko wa dharura ili kupunguza athari hizo kwa wananchi, hususan kupanda kwa gharama za maisha kama nauli na bei za bidhaa.



Chapisha Maoni

0 Maoni