Wanachama wa CCM mtufundishe wabunge kuwa bora- Biteko

Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, kuwafundisha wabunge wao kuwa Bora.

Dkt. Biteko ameyasema hayo Aprili 19, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Chama hicho Mkoa wa Geita, uliofanyika katika viwanja vya ofisi mpya za CCM Mkoa.

“Hakuna jambo la ajabu kuwa Mbunge bali Watanzania wamekupa Imani tu”. Dkt. Biteko ameongeza kuwa Mbunge bora na mbaya anatengezwa na wapiga kura wake, hivyo wasiache kuwakosoa pale wanapofanya vibaya ili wawe Bora zaidi.

Aidha, Dkt. Biteko amewaomba wabunge wa majimbo mengine ya Mkoa wa Geita, kuwaunganisha wananchi kwa kuwaweka katika uelekeo mmoja wa Maendeleo na sio kuwagawa makundi makundi.

Chapisha Maoni

0 Maoni