Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 26, 2026
anafanya ziara katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo amekagua maendeleo
ya ujenzi wa Daraja la Mkwajuni lenye urefu wa mita 20 na kimo cha
mita 5.5 ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni
11.6
Pia Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amekagua mradi wa ujenzi wa
Daraja la Kigogo lenye urefu wa mita 50 kimo cha mita 8.9 na barabara
unganishi zenye jumla ya urefu wa mita 625 ambalo hadi kukamilika
kwake litagharimu shilingi bilioni 17.7.





0 Maoni