Dkt. Mwinyi akutana na Kaimu Balozi wa Marekani kuimarisha ushirikiano

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Kaimu Balozi Wa Marekani Nchini Tanzania Balozi Andrew Lentz kuzungumzia Maeneo mbalimbali ya Ushirikiano baina ya Zanzibar na Marekani. 

Mazungumzo hayo Yamefanyika leo tarehe 23 Machi 2026 Ikulu , Zanzibar.

Rais DÄ·t. Mwinyi amemuelezea Kaimu Balozi lentz kuwa Zanzibar ina Mipango na Mikakati madhubuti ya Kuhakikisha inajitegemea yenyewe na kujitosheleza katika Masuala ya Nishati ya Mafuta ,Umeme na kuwa kituo Kikuu Cha Usafirishaji kupitia Bandari kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati. 


Rais DÄ·t. Mwinyi amesema Ujenzi unaoendelea wa Mradi wa Bandari jumuishi ya Mangapwani ni Mradi unaotarajiwa kumaliza Matatizo hayo na kwamba kasi ya Ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar Itaongezeka maradufu kutokana na Uwekezaji Mkubwa unaokwenda kufanyika katika Bandari hiyo ikiwemo Mitambo ya Uzalishaji wa Megawati 200 za Umeme, Kuwepo kwa Matangi ya Hifadhi ya Mafuta na Bandari itakayoweza kuhudumia Meli zenye Uwezo wa kubeba Makontena mengi zaidi na kumaliza tatizo la Msongamano wa Meli katika Bandari ya Malindi.


Amefahamisha kuwa Ukuaji wa Sekta ya Uwekezaji hapa Nchini na Utekelezaji wa Miradi mikubwa ya Maendeleo kumeilazimu Zanzibar kutafuta njia Mbadala za kuweza kujitegemea kwa Nishati ya Umeme, Mafuta na gesi pamoja na kuleta Mageuzi makubwa katika Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani.


Rais DÄ·t. Mwinyi ameihakikishia Marekani Ushirikiano zaidi katika nyanja mbalimbali na kuishukuru kwa Misaada ya Nchi hiyo kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar na kwamba kuna kila sababu ya kuendeleza Ushirikiano huo wa Muda mrefu. na kubainisha kuwa bado zipo fursa nyingi ambazo Makampuni na Wawekezaji kutoka Marekani wanaweza kuwekeza Nchini.


Naye Kaimu Balozi Andrew Lentz ameeleza kufarijika na hatua ya Maendeleo inayoendelea kufikiwa na Zanzibar hususan katika Ujenzi wa Miundombinu hatua aliyoielezea kuwa ni kipaumbele kwa Nchi inayohitaji Kuvutia Wawekezaji na Maendeleo ya Kiuchumi na Ustawi wa Watu wake na kuahidi kwa Nchi hiyo kuendelea kutanua Maeneo zaidi ya Ushirikiano na Zanzibar hususan katika sekta ya Afya , Mabadiliko ya Tabia Nchi, Biashara na Uwekezaji.




Chapisha Maoni

0 Maoni