Vijana wa Tanzania
wametakiwa kugeuza uzuri na utajiri wa nchi yao kuwa chimbuko la kuanzisha na
kujenga mahusiano yenye maana na tija kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Kauli hii inatokana na msemo wa Kiingereza unaosema, "Let her beauty be
the starting point of meaningful connections."
Wataalamu wa
maendeleo ya vijana na viongozi wa jamii wanasisitiza kuwa Tanzania imebarikiwa
kuwa na rasilimali nyingi kuanzia vivutio vya utalii, ardhi yenye rutuba, amani
na utulivu, mambo ambayo yanapaswa kutumika kama daraja la kuwaunganisha
vijana.
Badala ya uzuri wa
nchi kutazamwa tu kwa jicho la kitalii na kwa kupewa taarifa za kweli katika
upotofu, vijana wanahimizwa kuutumia utajiri huu wa kiasili na kiutamaduni ili
kusonga mbele.
Wataalamu hao
wanasema kwamba vijana wanaweza kutumia fursa za kimaumbile za nchi (kama vile
kilimo, utalii, na madini) kuanzisha ushirikiano wa biashara na miradi ya
pamoja. Mahusiano haya yanapaswa kuwa ya kujenga na kuongeza thamani kiuchumi.
" Utamaduni
tajiri na wa kipekee wa Tanzania unapaswa kuwafanya vijana wajisikie fahari na
kuungana zaidi. Mahusiano ya kijamii yanapaswa kujengwa kwa msingi wa upendo,
amani, na kuheshimiana, licha ya tofauti zao za kikabila au kidini."
Aidha vijana
wanatakiwa kuepuka mahusiano ya kindugu au yale yasiyo na tija yenye nia ovu
dhidi ya taifa lao na badala yake waelekeze nguvu zao katika kujenga mahusiano
ya kitaaluma, kijamii, na kisiasa yanayochochea maendeleo endelevu na ubunifu
kwa kutumia teknolojia zilizopo za mawasiliano.
Kiongozi mmoja wa
asasi ya vijana amesema, "Uzuri wa Tanzania unapaswa kutukumbusha kwamba
sisi ni ndugu. Tunapojenga mahusiano mazuri baina yetu, tunajenga mtandao ambao
utatuwezesha kupata masoko, mitaji, na maarifa ya kusaidiana kimaisha."
Kwa kutumia amani
na utulivu uliopo nchini, vijana wa Tanzania wanahimizwa kuona uzuri huu wa
nchi kama hatua ya kwanza katika kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio
kiini cha maendeleo yote.
Hivi karibuni
Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Nanauka, akiwa katika ziara ya mikoa
kadhaa nchini kuwasilikiliza vijana, amewataka vijana nchini kutumia utajiri na
uzuri wa Tanzania kama chimbuko la kujenga mahusiano yenye maana na tija.
Akizungumza maeneo mengi
amewaasa vijana kutumia amani na fursa za kimaumbile za nchi kuanzisha
ushirikiano wa biashara na miradi ya pamoja.
"Badala ya
kila kijana kujifungia kivyake, ni wakati sasa wa kuutumia uzuri wa nchi yetu
na amani iliyopo kuunda mitandao imara ya kitaaluma, kijamii na kiuchumi.
Mahusiano haya ndiyo yatawafanya vijana wawe wabunifu, wapate masoko, na hatimaye
kukuza uchumi wetu," alisema Waziri Nanauka.
Akizungumzia
utekelezaji wa wito huo, Sophia Mussa, kijana mjasiriamali anayejishughulisha
na usafirishaji wa mazao ya kilimo katika Mkoa wa Morogoro, amethibitisha
umuhimu wa kushirikiana:
"Mimi nimetumia
mitandao ya vijana wajasiriamali niliokutana nao kwenye vikao vya Serikali.
Bila amani na ushirikiano, nisingeweza kufikisha mazao yangu Dar es Salaam.
Mahusiano tuliyojenga kupitia fursa za nchi yametufanya tuwe na nguvu kubwa ya
kiuchumi."
Kwa kutumia amani
na utulivu uliopo nchini, vijana wa Tanzania wanahimizwa kuona uzuri wa nchi
kama hatua ya kwanza katika kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio kiini cha
maendeleo yote. Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka mazingira mazuri ya
kisheria na kiuchumi ili kuhakikisha vijana wanapata nafasi za kujiajiri na
kuajiriwa, huku ushirikiano baina yao ukionekana kuwa kiungo muhimu cha
kuendelea mbele.

0 Maoni