Serikali imetoa wito mzito kwa vijana kote nchini kutumia fursa za kimkakati za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) zilizopangwa na serikali, badala ya kurubuniwa na miito ya mtandaoni inayolenga kuvuruga amani na maendeleo ya Taifa.
Wito huu unakuja
wakati Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiongeza kasi ya
uwekezaji mkubwa kwa vijana katika sekta ya kidijitali.
Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb),
ameagiza kuongeza kasi ya ufunguaji wa ICT Hubs katika vyuo, shule za kata, na
maeneo ya jamii.
Waziri Kairuki
alisisitiza kuwa hatua hiyo ndiyo msingi wa kuandaa taifa lenye ujuzi wa
teknolojia na uwezo wa kushindana katika uchumi wa kisasa wa kidijitali.
"ICT Hubs ni
nguzo muhimu katika kujenga mazingira ya kujifunza, kubuni na kutengeneza
suluhu za kiteknolojia zinazohitajika katika maendeleo ya kijamii na
kiuchumi," alisema Waziri Kairuki.
Serikali
imejipanga kuhakikisha maendeleo ya TEHAMA yanakwenda sambamba na Ilani ya
Chama Tawala, inayosisitiza kuandaa na kutekeleza mikakati ya kutumia
teknolojia zinazoibuka kama vile:Akili Bandia (Artificial
Intelligence),setilaiti,blockchain na roboti
Elimu na Ubunifu Kwanza, Sio Vurugu
Waziri Kairuki
alisema upanuzi wa ICT Hubs utakuwa sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo wa
kitaifa.Ujuzi wa Kisasa: Kuwepo kwa ICT Hubs kutawasaidia wanafunzi kupata
ujuzi wa kisasa, ikiwemo coding, utengenezaji wa mifumo, uchambuzi wa data, na
matumizi ya roboti—stadi zinazohitajika katika soko la ajira la Karne ya 21.
Vijana wakipata nafasi ya kufanya majaribio na
kubuni bidhaa za teknolojia wakiwa bado shuleni, taifa litazalisha wataalamu
wenye uwezo mkubwa wa ubunifu na kutatua changamoto kwa kutumia maarifa ya
TEHAMA, badala ya kuchoma nchi yao kupitia mitandao.
Aidha ICT Hubs
zitachangia kupunguza pengo la kidijitali kati ya mijini na vijijini kwa
kuwawezesha wanafunzi na walimu kupata vifaa na mtandao madhubuti.
Katika kuimarisha
mazingira ya uwekezaji na ubunifu, Waziri Kairuki ameiagiza Tume ya TEHAMA
kuanzisha majukwaa ya uwekezaji yatakayowakutanisha wabunifu, sekta binafsi,
taasisi za Serikali, na wawekezaji.
Majukwaa haya
yanalenga kusukuma mbele miradi ya teknolojia ikiwemo ile ya akili unde na
mifumo salama ya kidijitali.
"Majukwaa
hayo yatachochea ushirikiano na kuongeza mtandao wa fursa kwa vijana
wanaotengeneza bidhaa za kiteknolojia," alieleza Waziri Kairuki.
ICT Hubs (Vituo
vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) ni zaidi ya maabara za kompyuta; ni
mfumo kamili wa kuwezesha vijana kugeuza mawazo yao kuwa biashara halisi za
kidijitali.
Njia kuu ambazo
ICT Hubs huongeza fursa za ujasiriamali wa kidijitali kwa vijana kuwa kupata
maarifa na ujuzi maalum (Skills Acquisition)ICT Hubs hutoa mafunzo yaliyolenga
soko la kimataifa, tofauti na elimu ya kawaida ya darasani:Pia kuna kuongeza
umahiri wa Coding (Programming): Vijana hujifunza lugha za programu (kama
Python, JavaScript, n.k.) zinazohitajika kuunda tovuti, programu za simu, na
mifumo mbalimbali.
Pia ICT Hubs
husaidia vijana kupata ujuzi wa kukusanya, kuchambua, na kutumia data kusaidia
biashara kufanya maamuzi sahihi—ujuzi unaoongoza katika uchumi wa kisasa.
Hubs hutoa mafunzo kuhusu teknolojia
zinazoibukia, ambazo ndio msingi wa bidhaa na huduma za kipekee za siku
zijazo., Kuendeleza Mawazo na Prototypes (Idea Incubation)Vituo hivi hufanya
kazi kama Incubators na Accelerators, vikiwapa vijana rasilimali muhimu za
kuanzisha biashara:
Mkulima au mwalimu
kijijini anapata fursa ya kujifunza jinsi ya kutumia teknolojia kuboresha kazi
yake, akitumia Hub iliyo karibu naye na hivyo kumwezesha kutengeneza suluhu za ndani:Kwa kifupi, ICT
Hubs zinatoa vifaa, elimu, ushauri, na masoko mambo yote ambayo kijana
anahitaji ili kuanza safari yake ya ujasiriamali wa kidijitali bila kutegemea
ajira za serikali.

0 Maoni