Picha za CCTV na kumbukumbu za vurugu zilizotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, zimebakia kuwa somo chungu na wito wa dhati kwa Taifa: Vitendo vya uharibifu na uchochezi havipaswi kujitokeza tena. Serikali, wadau wa maendeleo, na vijana wenyewe wanasisitiza kwamba uharibifu wa mali na ukiukwaji wa utu hauna nafasi katika Tanzania inayoendea uchumi wa kati wa juu.
Katika kila kumbukumbu ya tukio la kutisha
la Oktoba 29 wito unatolewa na vijana wenyewe wakisisitiza kwamba jukumu la
kulinda amani linaanzia kwao, kwa kutambua kuwa maendeleo hayawezi kustawi kama
kuna moto wa chuki na mgawanyiko.
“Amani si tu ukosefu wa vita, bali ni
hali ya utulivu, heshima, na umoja inayotuwezesha kujenga pamoja.” – Kauli ya
Vijana Wanaopenda Amani.
Ujumbe huu unasisitiza misingi mikuu
ya kuepuka kurudia makosa ya zamani kwa kila Mtanzania ni Balozi wa Amani.
Wengi wamekiri kuwa umaskini hauwezi
kuisha kwa siku moja, lakini amani inaweza kuisha kwa siku moja na kuleta tabu
kubwa kuirudisha. Vijana wanahimizwa kutokubali 'njaa na matumbo' viwaongoze
kufanya ujinga wa aina hii.
Dira ya Taifa ya Tanzania 2050
imeweka wazi maono ya nchi yetu kuwa kitovu cha viwanda katika Ukanda wa Afrika
Mashariki na Kusini. Lengo hili la kufikia Uchumi wa Kati Ngazi ya Juu, wenye
pato la mtu mmoja la Dola za Marekani $7,000 kwa mwaka, linatekelezeka tu chini
ya mazingira ya amani na utulivu.
Maono haya makubwa yanakinzana moja
kwa moja na vitendo vya kihujuma kama vile kuharibu miundombinu iliyojengwa kwa
kodi za walipa kodi, kuiba mali za wananchi, na kuvuruga maisha ya watu wasio
na hatia. Vitendo kama hivyo vinaelezwa kuwa ni uhujumu wa uhuru wetu na
kujaribu kuirudisha nyuma Tanzania iliyojengwa kwa miaka mingi.

0 Maoni