Baada ya Tanzania kutajwa na mtandao wa World Travel Awards kama nchi inayoongoza kwa Utalii wa Safari mwaka 2025 imekuwa ni chachu ya kutangaza mazao mapya ya Utalii katika soko la Dunia yanayopatikana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayeshughulikia huduma
za utalii ambaye yupo Bahrain ambapo hafla ya utoaji wa tuzo za WTA zimeanyika
amesema Ngorongoro ina nafasi kubwa
kimataifa kuuza mazao mapya ya utalii duniani kutokana na kukua kwa sekta ya
utalii.
Tanzania imetunukiwa tuzo hiyo adhimu katika sekta
ya utalii duniani wakati wa hafla ya 32
ya World Travel Awards (WTA) iliyofanyika katika ukumbi wa Exhibition World
Centre nchini Bahrain tarehe 6 Desemba, 2025 .
Akizungumza baada ya Hafla hiyo Kamishna Kobelo
ameeleza kuwa kufuatia ushindani wa tuzo
za utalii katika nyanja mbalimbali Tanzania hususan eneo la hifadhi ya
Ngorongoro itaendelea kuboresha miundombinu ya utalii na kutangaza mazao mapya
ya utalii hasa utalii wa Makumbusho Jiopaki
ya Ngorongoro Lengai na Olduvai pamoja na vivutio vya urithi wa
utamaduni na mambo kale ili yafahamike zaidi na kuweza kushindanishwa kidunia.
Kobelo ameeleza kuwa Tanzania ni sehemu salama na
ina vivutiio vingi ambavyo vinapaswa kupelekwa soko la Kimataifa na kuendelea
kupokea wageni wengi na pato la Taifa kuongezeka ili kuendeleza matokeo chanya
ya Filamu ya Tanzania the Royal tour na Amaizing Tanzania.
Nchi ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tuzo
za utalii duniani mwaka 2026 ambapo wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mataifa
mbalimbali ulimwenguni watashiriki.




0 Maoni