Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha mafunzo ya Uongezaji thamani madini ya vito kwa kuongeza nguvukazi na kufanya kazi kwa masaa 24 ili kukamilisha ujenzi wa jengo kwa muda mfupi.
Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 12, 2025
mkoani Arusha wakati wa ziara yake
ya kukagua mradi wa kituo hicho ulioanza ujenzi rasmi ambapo katika maelekezo
yake amemtaka mkandarasi kuzingatia ujenzi bora wenye kukidhi vigezo
vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya
Sita inayoongozwa na Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza mikakati yake
kwenye mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini ya vito kama Sera ya Madini
ya Mwaka 2009 inavyoelekeza.
Sambamba na hapo, Waziri Mavunde amesisitiza kuwa, kuanza
kwa ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Mhe. Rais. Dkt.
Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia Bunge la 13 jijini Dodoma.
Waziri Mavunde amebainisha kuwa, kukamilika kwa kituo hicho , kutaleta faida mbalimbali ikiwa
pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi watakao jiunga kwenye kituo,
kuongezeka kwa wataalamu wa uongezaji thamani madini ya vito, kufungua fursa za
ajira kwa vijana na wafanyabiashara wa madini , pamoja na kutosafirishwa kwa
madini ghafi nje ya nchi hivyo kutachagiza
ongezeko la mapato kwa taifa.
Kwa upande wake , Mkuu wa Wilaya Arusha Mhe. Joseph
Mkude ameahidi kuendelea kufuatilia maendeleo ya ujenzi ili kuhakikisha ujenzi
unakamilika kama Serikali inavyotaka.
Mkude ameongeza kuwa, kukamilka kwa kituo hicho
itakuwa moja ya sehemu ya uwekezaji mkubwa wa serikali husasan kwenye Sekta ya
Madini mkoani Arusha.
Awali, akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi, Mkuu
wa kituo cha TGC Mhandisi. Ally Maganga ameeleza kuwa, ujenzi wa majengo pacha
hayo ya ghorofa 8 utagharimu Tsh Bilioni 33 na kukamilika kwake kutaongeza
fursa ya vijana wengi kupata ajira kupitia ujuzi wa uongezaji thamani madini ya
vito.
Naye Meneja Mradi Mhandisi Robert Lubuva ameahidi
kuhakikisha kama wakandarasi wataongeza nguvu ya rasilimali watu na vifaa ili
mradi uweze kukamilika na kuwahudumia watanzania kwa wakati.
#MadiniNiMaishaNaUtajiri
Asilimia10.1GDP
UongezajiThamaniMaendeleoyaTaifa



0 Maoni