Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya
kimataifa kama “Nchi Inayoongoza Duniani kwa Utalii wa Safari” katika Hafla ya
Fainali za World Travell Awads 2025.
Tanzania imetunukiwa taji hili adhimu katika Sekta
ya utalii duniani wakati wa Hafla ya 32 ya World Travel Awards (WTA 2025),
iliyofanyika katika Ukumbi wa Exhibition World Center nchini Bahrain tarehe 6
Desemba 2025.
Tuzo za WTA, zinazotajwa kama “Tuzo za Oscars za
utalii duniani” kutokana na hadhi yake kubwa katika Sekta, Tuzo hizi zimewaleta
pamoja zaidi ya washiriki 500 wakiwemo viongozi wa Serikali na wadau wa utalii.
Tanzania
imeshinda Tuzo nne miongoni mwao ni Kisiwa mashuhuri cha Zanzibar (Spice
Islands) kushinda Tuzo ya World MICE Awards 2025 kama “Eneo Bora Afrika kwa
Mikutano na Matukio ya Kitaasisi.”
Halkadhalika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,
imetangazwa kuwa “Hifadhi Bora ya Taifa Duniani 2025” katika tuzo hizo za WTA.
Aidha, Tanzania imepata tuzo mbili zaidi katika
kundi la Sekta Binafsi, ikiwemo “Kampuni Bora ya Safari za Puto Duniani,”
iliyotwaliwa na kampuni ya Serengeti Balloon Safaris.
Tuzo nyingine imekwenda kwenye Kisiwa bora cha
Mapumziko Duniani na Jumaira Thanda
Resort katika Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania imeibuka mshindi katika
kipengele hicho.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo za WTA,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema tuzo
hizo ni uthibitisho wa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na
sekta binafsi katika kukuza utalii endelevu na kuimarisha uhifadhi nchini.
Tanzania, ambayo imeshinda tuzo kwa mwaka wa pili mfululizo, inatarajiwa kuwa
mwenyeji wa hafla ya fainali ya World Travel Awards
itakayofanyika Desemba 2026.



0 Maoni