Katika hatua
inayoungana na wito wa amani, mfanyabiashara wa mitandaoni, Jennifer Jovin
(Niffer), ambaye hivi karibuni alipata msamaha wa Rais na kuachiwa huru, ameapa
kuwa balozi wa vijana ili kulinda mienendo ya vijana dhidi ya ushawishi wa
vurugu na uharibifu.
Niffer
amewakumbusha vijana kwamba kuna makosa mengi wanayofanya bila kujua ambayo
yanapelekea hasara kubwa kwa jamii na familia. Alitoa mfano wa vurugu za Oktoba
29 zilizosababisha upotevu wa mali na maisha.
"Nitakuwa
balozi mzuri wa vijana wenzangu, kuweza kulinda mienendo yetu, tunaishije,
tunafanyaje na tunaepuka kipi na tunafanya kipi kwa wakati sahihi,"
amefafanua Niffer.
Niffer kwa kauli
yake anaungana na serikali na wadau wengine wanaotambua kwamba Tanzania
imebarikiwa kuwa kisiwa cha amani. na anawahimiza vijana wenzake kutunza urithi
huu kwa gharama yoyote.
Aidha katika
mazungumzo yake ametahadharisha kauli au matendo yanayolenga kuleta tafarani ya
kitaifa.
Anahimiza wajibu
wa kutunza na kuilinda miradi ya
maendeleo inayotekelezwa kwa kodi za wananchi na inafaa vizazi vijavyo. Ni
wajibu wa vijana kuitunza, sio kuichoma kwa ajili ya ajenda za watu wenye nia
mbaya na Taifa.
Tanzania
inawahimiza Watanzania wote kuendelea kuijenga nchi kwa umoja na utulivu, bila
kuruhusu wajanja wa mitandaoni kuigeuza nchi kuwa sehemu ya machafuko kwa
maslahi yao binafsi.

0 Maoni