Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema serikali
imeendelea kufanya mikutano na viongozi wa taasisi mbalimbali za dini, ikiwemo
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), na viongozi wa kimila ili kuwaeleza
hali halisi ya usalama nchini na kuwataka kuendelea kudumisha amani.
Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi wa Arusha katika ziara
byake ya kikazi ambayo poia ameitumia kuangalia uharibifu uliofanywa katika
vurugu ya Oktoba 29.
Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa amani kama msingi mkuu wa maendeleo ya
taifa.
Katika ziara hiyo pia aliwapa
wananchi salamu za pole zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia
athari za vurugu zilizotokea hivi
karibuni.
Waziri Mkuu alitembelea na kukagua uharibifu uliotokea wakati wa vurugu
za Oktoba 29, 2025, ambapo Kituo cha Polisi cha Kikatiti, Mahakama ya Mwanzo ya
Maji ya Chai, na kituo cha mafuta cha Total Energies vilichomwa moto. Aidha,
alibaini kuibwa kwa mali katika soko kuu na kubomolewa kwa sefu ya kutunzia
fedha.
Waziri Mkuu amewaonya wananchi kuwa kuchagua vurugu ni sawa na kuchagua
kufukuza maendeleo na kuongeza umaskini kwa mtu mmoja mmoja, akisisitiza kuwa
ahadi za maendeleo kama maji na barabara zitafanyika endapo tu nchi itakuwa na
amani.

0 Maoni