Baada ya matukio yaliyotokea Oktoba 29, 2025, kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC), Mchungaji Anthony Lusekelo (‘Mzee wa Upako’), ametoa wito kwa Watanzania kutafakari na kujifunza kutokana na tukio hilo, akieleza kuwa lilitikisa sana heshima ya Taifa na halipaswi kurudiwa kamwe.
Kauli hii inatolewa huku Wito wa
Kitaifa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kulinda amani ukiendelea kusambaa
kwa kasi miongoni mwa wananchi na vijana.
Mchungaji Lusekelo ameeleza kuwa
tukio hilo limekuwa uzoefu mchungu ambao Watanzania hawakuwahi kuupitia,
akifananisha hali iliyotokea Oktoba 29 na "vita ya wenyewe kwa
wenyewe," na kulifananisha na mazingira ya vita ya 1977/1978 dhidi ya Idd
Amin.
Akitoa pole kwa wakazi wa Dar es
Salaam, Arusha, Songwe na Mwanza walioathirika, amesisitiza kuwa hali hiyo
iligusa Watanzania bila ubaguzi, akitaja hata baadhi ya waumini wake maeneo ya
Kimara waliathirika.
Alisema ipo haja viongozi wa
dini, wazazi, viongozi wa serikali na kisiasa kutafakari namna heshima ya nchi
ilivyotikisika na umuhimu wa kurejea kwenye misingi ya umoja na ustaarabu.
Amewaonya Watanzania kuwa ni
muhimu yale yaliyotokea yakawa funzo, kwani huenda Taifa likakumbana na tukio
kubwa zaidi baada ya miaka michache ijayo endapo amani haitalindwa.
Maoni haya ya viongozi wa dini yanaungana
na msimamo thabiti wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alitoa
wito kwa Watanzania wote kulinda amani.
"Serikali Haitaruhusu Nchi
Ivurugwe: Tutailinda Nchi kwa Nguvu Zote."
Wito huu umeelekezwa hasa kwa
vijana, kuwakumbusha kuwa Amani ndiyo mtaji mkuu wa elimu, ajira, na biashara
yao. Wamehimizwa kukataa kauli yoyote yenye nia ya kutugawa au kuvuruga utulivu
tulionao.
Kauli za wananchi zilizotolewa
mtandaoni baada ya tukio zinaonesha jinsi ujumbe huu unavyopokewa:Kujifunza na
Kusamehe: Raia wengi wanakubaliana kwamba, "Ni kuelewana tu, tukikaa chini
kila kitu kitakuwa sawa," huku wakisisitiza: "Tujitolee kusamehe,
lakini tusisahau umuhimu wa kujifunza kutoka kwa makosa ya zamani."
Wananchi wamehimiza kuwa amani
lazima idumishwe, lakini iambatane na haki kwa kila Mtanzania.
Ujumbe wa Rais umeeleza wazi kuwa kulinda nchi
si kazi ya vyombo vya ulinzi pekee: "Ni jukumu la kila mmoja wetu, tukiwa
na uzalendo na upendo kwa Taifa letu. Tuwe walinzi wa Amani katika familia,
vitongoji, na maeneo yetu ya kazi."

0 Maoni