Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Desemba 2, 2025
amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni mama ya
Perseus na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga, Bi. Lee-Anne de Bruin ambao
ni wawekezaji kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilayani
Sengerema. Bi. Lee-Anne de Bruin aliongozana na Bw. Matt Cavedon, Meneja Mkuu
na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga na Bw. Isaac Lupokela, Afisa Mkuu wa
Fedha wa Mradi wa Nyanzaga.
Mazungumzo hayo yaliangazia hatua mbalimbali zilizofikiwa
katika utekelezaji wa uanzishwaji wa mgodi huo ambao unatarajiwa kuwa na
mchango mkubwa kwenye uchumi wa Nchi yetu na wananchi wa Sengerema.
Aidha, Waziri Mavunde aliwahakikishia wawekezaji wa Perseus
kuwa Wizara itaendelea kuwa bega kwa bega na wawekezaji katika kufanikisha
uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa Nyanzaga ili uweze kuleta mafanikio kwenye
uchumi wa Tanzania na kusaidia upatikanaji wa Ajira kwa Watanzania wengi.
#InvestInTanzania
#Vision2030: Madini ni Maisha&Utajiri

0 Maoni