Kumekuwa na wito
kwa Watanzania kutafakari kwa kina kauli za uchochezi zinazoenezwa na baadhi ya
watu kupitia mitandao ya kijamii, hususan kutoka kwa anayejiita mwanaharakati
Mange Kimambi anayeishi nchini Marekani.
Wito huo unafuatia
kauli za hivi karibuni za mwanamama huyo ambaye amekuwa akiwahimiza Watanzania
kushiriki maandamano na vurugu nchini, huku akijitenga wazi na wazo la kuja
kushiriki yeye mwenyewe.
Katika posti zake
za mitandaoni, mwanamama huyo alifanya dhihirisho la wazi la kutokukabiliwa na
matatizo yoyote , akijinadi kuwa hana sababu ya kuja kushiriki maandamano.
Alijiuliza: "Mimi nateseka kitu gani na CCM mpaka nitoke Marekani nije
mtaa? Nateseka namna gani?"
Alikiri waziwazi
kufurahia maisha mazuri nchini Marekani, akitaja kuishi katika nyumba ya
kifahari, kuendesha biashara inayomwingizia kipato, pamoja na kufurahia huduma
za uhakika kama vile mfumo wa afya wa dharura wa 911 na kutokatika kwa umeme.
Kauli hizi zimezua
maswali mazito kutoka kwa wachambuzi na Watanzania wa kawaida: Je, kweli mtu
anayeishi katika "pepo" ya kisasa, iliyojengwa kwa miaka 300 kwa
utulivu na kazi, ana nia njema na Watanzania anaowashauri kuharibu miundombinu
na kuhatarisha maisha yao?
Wito wa Kutafakari
na Kukataa Uchochezi
Wachambuzi wa
masuala ya kijamii wanasema kauli za Mange Kimambi ni dhihirisho la wazi kwamba
yeye anainjoi matunda ya nchi iliyotulia, yenye sheria, na iliyostawi, huku
akiwataka wengine wateseke kwa ajili ya ajenda zake binafsi.
"Huyu ni
kivuruge na mchochezi. Anawaza uharibifu huku yeye akifurahia usalama na amani
ya Marekani," alisema mmoja wa wachambuzi. "Anatumia nafasi yake ya
kuishi maisha mazuri kuwafanya Watanzania wa hali ya chini kuwa 'kete' katika
mchezo wake wa kisiasa. Kila mtu anayeandika 'Njoo tuandamane!' akikwepa kuja
yeye mwenyewe ni kinara asiye na shida wala ajenda ya dhati."
Watanzania
wamehimizwa kufikiri kwanza na kuepuka kuwa daraja la kivuruge kufikia malengo
yake ya kibinafsi.
Wito umekuwa ni
kulinda amani ambayo haina bei, badala ya kuharibu miundombinu na mustakabali
wa watoto kwa ajili ya maneno ya mtu anayeishi mbali na matatizo yao. Badala ya
kubomoa, Watanzania wametakiwa kutumia nguvu na akili zao kujenga nchi yao,
kwani nchi zilizostawi hazikujengwa kwa vurugu bali kwa kazi ngumu na utulivu.
"Tupinge
kauli za uchochezi kwa kuthamini maisha yetu na Taifa letu kwanza. Haturuhusu
mtu yeyote atumie nchi yetu kama uwanja wa michezo kwa masilahi yake
binafsi," inahitimisha kauli hiyo.

0 Maoni