Amani siyo maneno
ni kazi. Vijana tukisimama pamoja, Tanzania inang'aa zaidi! Kaulimbiu hii
imepata nguvu mpya baada ya Kampuni ya Meta, wamiliki wa majukwaa makubwa ya
mitandao ya kijamii, kuchukua hatua madhubuti ya kuzifunga akaunti za watu
wawili maarufu kwa uchochezi na uvunjifu wa amani nchini Tanzania: Mange
Kimambi na Maria Sarungi Tsehai.
Hatua hii
imepokelewa kwa shangwe na Watanzania wanaopenda amani, kwani inaonekana kama
ulinzi wa moja kwa moja dhidi ya mipango ovu iliyokuwa ikipangwa kupitia
majukwaa hayo.
Kwa mujibu wa
wachambuzi wa masuala ya usalama na jamii, akaunti hizi zilikuwa zimegeuzwa
kuwa "ghala la fitina" na "kiwanda cha chuki". Walibainisha
kuwa badala ya kutumika kwa mawasiliano ya kujenga, wamiliki wake walizitumia
kama silaha za kisiasa zenye malengo ya kueneza uvumi na habari za uongo,zisizo
na uthibitisho;Uchochezi wa kuingia mitaani wakihimiza umma kuingia mitaani
bila sababu za msingi na kupora huku wakishirikiana na vikundi vya nje na
mashirika yenye ajenda za siri zinazolenga kuvuruga uchumi na amani, wakiwa na
silaha nyingine ya matumizi ya lugha chafu huku wakitukana viongozi wa taifa na
taasisi za dola bila kuheshimu sheria.
Kufungwa kwa
akaunti hizi hakuna maana ya "uminyaji wa uhuru wa kujieleza" bali ni
hatua ya kuwawajibisha wale waliovuka mipaka ya uhuru na kuingia kwenye uhalifu
wa moja kwa moja kama uchochezi, uenezi wa chuki na mipango ya kigaidi ya
kisiasa. Uhuru wa kweli huja pamoja na wajibu wa kulinda amani na umoja wa
Taifa.

0 Maoni