Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Dodoma limetoa hadhari makundi mitandaoni yanayochochea vurugu, huku likisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Mwenyekiti wa BAKWATA, Wilaya ya Dodoma, Sheikh Bashiru
Ghazali, akizungumza kwa uzito, amesema makundi haya yanatumia mitandao kwa nia
ya "kusababisha ubaguzi dhidi ya viongozi na serikali".
Anasema, "Hali ni mbaya sana na kuna hatari ya kupokea
kwa usalama kutokana na harakati za makundi yenye vikundi" vinavyoeneza
chuki na upotoshaji. Sheikh Ghazali aliongeza kuwa ni jukumu la Watanzania kuheshimu na kulinda uhuru wa dini.
Kauli hii inalingana na maoni ya wananchi. Mzazi Aisha
Kayuni wa Mbeya anayesisitiza kuwa, “Taasisi za kiserikali hazipaswi kutoa
fursa kwa taasisi za kidini kuhubiri na kuonesha chuki, uhasama wala kuwalaumu
waumini wao”.
Wananchi wanaaswa kuwa makini na kuepuka kufuata ajenda za
vikundi hivi.
Mzazi Samwel Ali anatoa wito, akisisitiza “amani ndio
chanzo cha furaha na ustawi wangu binafsi”. .
Hivi karibuni Waziri
wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amesikika akisema inapaswa kuwa na
kengele ya kuamsha kila kijana wa Kitanzania anayeipenda Nchi hii akitafakari
methali isemayo, "Akipenda chongo, huita kengeza," lakini linapokuja
suala la amani ya nchi, hatuna anasa ya kujidanganya.
Akirejea mfano wa jirani zetu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), Waziri alituonyesha picha halisi na ya kutisha: Taifa ambalo
limekuwa kwenye migogoro kwa zaidi ya miaka 30. Vijana wa huko, ambao leo ni
wazee, wamepoteza maisha yao yote wakitafuta amani ambayo walichezea miongo
mitatu iliyopita.
Kwa kijana "Gen Z" unayesoma hapa: Hii amani
tuliyonayo siyo zawadi, ni jukumu. Wale wanaokushawishi uingie barabarani
kubomoa maduka na kuchoma matairi hawatakuwepo wakati uchumi unaporomoka.
Hawatakuwepo wakati mama lishe anashindwa kuuza chakula au bodaboda anashindwa
kupata abiria kwa hofu ya usalama.
Tanzania ni kisiwa cha amani katika bahari iliyojaa
dhoruba. Tumeona kilichotokea Sudan, tumeona Kongo. Njia ya mkato ya vurugu
haijawahi kumfikisha mtu kwenye neema. Njia pekee ya kweli ni ile ya
kujenga,kujenga hoja mezani, na kujenga taifa kwa kufanya kazi.
Tusiingize nchi
kwenye umwagaji damu kwa majaribio yasiyo na tija. Amani ni kama afya;
ukiipoteza, ndipo utajua thamani yake. Tuitu

0 Maoni