Amani na utulivu wa nchi ni msingi mkuu unaowezesha mafanikio ya jitihada zote za Serikali, ikiwemo uwekezaji mkubwa unaofanywa katika sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Bila amani, mageuzi yanayolenga kuwapa vijana ujuzi wa kitaalamu na wa kidijitali hayawezi kushamiri na kuleta tija katika soko la ajira.
Hii ndio sababu amani ni nguzo kuu
kwa Teknolojia kushamiri na kuwanufaisha vijana:
Miundombinu ya Kitaaluma
Uwekezaji mkubwa unaofanywa na
Serikali, ikiwemo ujenzi wa vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi
(Polytechnics) katika mikoa mbalimbali, unahitaji mazingira salama ili ijengwe,
iendeshwe, na itumike kwa ufanisi.
Matumizi ya TEHAMA:
Amani inahakikisha shule, vyuo, na
miundombinu ya TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) haiwezi kuvurugwa
au kuharibiwa kutokana na machafuko, hivyo kuruhusu vijana kupata ujuzi wa
Digital Literacy na Critical Thinking kwa uendelevu.
Uwekezaji wa Nje (Diaspora na Washirika)
Serikali imeanzisha mikakati ya
kuongeza mchango wa Watanzania wanaoishi nje (Diaspora) katika kutoa utaalamu,
mbinu za kisasa za ufundishaji, na kuongeza fursa za ushirikiano na taasisi za
ndani, amani ndio itawezesha hilo.Itambulike kuwa wachangiaji wa nje
(wataalamu, wawekezaji, na Diaspora) wanavutiwa kuleta maarifa, ubunifu, na
mitaji yao tu katika nchi yenye amani, ambapo wanajua uwekezaji wao utakuwa
salama na utaweza kuzaa matunda.
Akili unde (AI):
Amani huwezesha ushirikiano katika
maeneo magumu kama Akili unde (AI), kusaidia kuandaa vijana kwa ajira katika
uchumi wa kidijitali.
Ushirikiano Kati ya Vyuo na Viwanda
Moja ya malengo ya Serikali ni kukuza
ushirikiano kati ya vyuo vya elimu ya kati/juu na sekta ya viwanda, ili
kuhakikisha wahitimu wanapata ujuzi unaohitajika sokoni.Kiukweli amali na ujuzi
wa kiteknolojia unaohitajika katika sekta ya fedha, simu na serikali unahitaji
kuwepo kwa viwanda na makampuni yanayofanya kazi kwa utulivu na kuaminiana.
Amani hutengeneza mazingira ya biashara na uzalishaji, ambapo vijana wanaweza
kuajiriwa au kujiajiri (kwa kuanzisha kampuni zao).
Dira 2050:
Waziri Mkenda amesema mipango
inalenga kujenga rasilimali watu bora, nguzo muhimu ya kufikia malengo ya DIRA
2050. Amani ni chachu muhimu katika kufikia dira hiyo.
Kwa ufupi, amani ndiyo jukwaa ambalo
juu yake uvumbuzi, uwekezaji, na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali yanaweza
kusimama, na hivyo kumuandaa kijana wa Kitanzania kuwa rasilimali watu yenye
uwezo wa kushindana kimataifa.

0 Maoni