Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeungana na Jamhuri
ya Kenya kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya uhuru wa Taifa hilo
(Jamhuri Day), zilizofanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Katika sherehe hizo Tanzania imewakilishwa na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe.
William Lukuvi (Mb) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tanzania na Kenya zina uhusiano wa kidugu na
kihistoria ambao umedumu kwa muda mrefu na unaendelea kuimarika siku hadi
siku. Nchi hizi mbili zimekuwa
zikishirikiana katika nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, usalama, utamaduni
na kijamii na pia katika ngazi za Kikanda na Kimataifa, hususan kupitia Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja
wa Mataifa (UN).



0 Maoni