Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake kwa kuwapa mafunzo ya namna bora ya kusimamia masuala ya Itifaki na kuhudumia wageni mbalimbali wanaotembelea hifadhi hiyo.
Akifungua mafunzo kwa Maafisa Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka
hiyo jijini Mwanza Mshauri wa
Jeshi la Uhifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya ameeleza kuwa ni muhimu kwa
kwa maafisa uhusiano kwa umma wa mamlaka hiyo kuendelea kujiimarisha katika
masuala ya mawasiliano na itifaki za kijeshi ili kuimarisha utendaji kazi wao
na kufikia viwango ambavyo mamkala imejiwekea kwenye mipango yake.
“Tunataka kuendelea kuwa Premium Safari Destination
katika taasisi yetu, hivyo ni muhimu kubadilika na kupeana mafunzo ya mara kwa
mara kwa kuzingatia ubunifu, maarifa na nidhamu maeneo ya kazi ili wageni
tunaowahudumia wafurahie huduma zetu na kuendelea kututangaza maeneo yote
duniani”alisema Kanali Machibya.
Kaimu Meneja Uhusiano kwa Umma wa Mamlaka hiyo Hamis
Dambaya amesema kuwa kufanyika kwa mafunzo hayo yeye na timu yake kutasaidia
kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho katika kipindi hiki ambacho mamlaka
hiyo imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa kiutendaji na kihuduma.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa
kivutio bora barani Afrika kutokana na umahiri wake katika kusimamia shughuli
zote za uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii jambo ambalo limekuwa likivutia
wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio vya
utalii vilivyopo.

0 Maoni