Hatua za Serikali za kuunda Tume
Maalumu ya kuchunguza vurugu zilizotokea nchini zimepokelewa kwa matumaini na
wachambuzi, huku wakisisitiza kuwa jukumu la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama
"Comforty Mkuu" wa Taifa ndilo litaleta uponyaji wa kweli.
Wakili na Mchambuzi wa Masuala ya
Kijamii, Emmanuel Ukashu, ameeleza kwamba hotuba ya Rais Samia ya kufungua
Bunge la 13 imetoa mwelekeo bora kabisa wa uponyaji wa Taifa katika majira haya
magumu.
Akichambua hali ya kisiasa kabla
na baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025, Wakili Ukashu alifafanua:“Unajua
kilichotokea ni matokeo lakini tayari huko nyuma haya mambo yalikuwa yanaonywa,
kwa sababu tumepitia nyakati ngumu kama Taifa. Nchi imevimba, na nchi ili iweze
kuwa na muafaka lazima watu tukae chini tuzungumze,” alisisitiza Wakili Ukashu.
Anasisitiza kuwa hotuba ya Rais
imekuwa muhimu sana kwa sababu inalenga kuleta muafaka wa kitaifa unaoanza kwa
Taifa kujitambua na kujitegemea kifikra, kisha kuunda mazingira ya mazungumzo.
Rais Samia: “Comforty Mkuu” wa
Taifa
Kwa Wakili Ukashu, katika nyakati
ambazo Taifa limepitia wakati mgumu, Rais Samia ndiye amekuwa comforty mkuu
(mfariji mkuu), ambaye hotuba yake imetoa mwelekeo wa uponyaji.
Katika hotuba yake, Rais Samia
alitoa wito wa maridhiano na umoja, akiahidi kuendelea kunyoosha mkono kwa
wadau wa kisiasa. Alitangaza kuwa Tume Maalumu imeundwa kuchunguza chanzo cha
vurugu hizo na kwamba ripoti yake itatumika kama mwongozo wa hatua za kuelekeza
Taifa kwenye amani ya kudumu. Pia, alitoa msamaha kwa vijana waliofuata mkumbo
wa uhalifu.
Hatua hizi za Rais, hasa uundwaji
wa Tume ya Uchunguzi, zinalenga kutibu majeraha ya kijamii na kuimarisha
misingi ya amani, sambamba na kuheshimu utu wa kila Mtanzania.
Ushauri wa Tume ya Maridhiano
Kama sehemu ya mwelekeo wa
uponyaji wa taifa, Wakili Ukashu alishauri kwamba mbali na Tume ya uchunguzi,
Taifa linahitaji Tume ya Maridhiano .
Alipendekezi kuwa tume ya
uchgunguzi inafaa majaji kuwepo, ipewe muda wa kutosha wa kufanya utafiti wa
kina kuhusu kiini cha vurugu hizo na taarifa yake iwekwe wazi kwa umma ili
kuanzisha misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Mapendekezo ya Wakili Ukashu
yanaonekana kuendana na dhamira ya Rais Samia ya kuanza mchakato wa Katiba Mpya
kwa kuanzisha Tume ya Usuluhishi na Maelewano, ikionyesha Serikali iko tayari
kukaa chini kuzungumza na wadau wote.
Kwa ujumla, wachambuzi wanaona hotuba
ya Rais Samia imefungua ukurasa mpya wa maridhiano, uwazi, na uponyaji, huku
ikisisitiza kuwa safari ya kuelekea amani ya kudumu inahitaji ushiriki wa kila
Mtanzania.

0 Maoni