Baada ya taharuki, hatua muhimu ni kuanzisha
mchakato wa Maridhiano ya Kitaifa. Lengo ni kuwezesha jamii, kisiasa, na kidini
kuketi pamoja, kujadili maumivu, kusamehe, na kuahidi kusonga mbele kwa pamoja.
Mifano ya kimataifa inaonesha faida za maridhiano ni
Afrika Kusini ilitumia Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) kuponya majeraha ya
ubaguzi wa rangi, na Rwanda (baada ya mauaji ya kimbari) imejenga upya Taifa
lake kwa misingi ya umoja na maridhiano.
Mmmoja wa wanasiasa Mkongwe anasema: "Maridhiano siyo kuficha
matatizo, bali ni kuyajadili kwa uwazi na upendo, na kuamua kwa pamoja kuwa
hatutaruhusu kugawanywa tena." Maridhiano yanahitaji utashi wa kisiasa na
utulivu wa kimoyo. Wananchi wanataka kuona viongozi wao wakionyesha mfano wa
kuweka tofauti za kando na kuungana.
Wananchi wanatoa kauli hizo wakati tayari Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua
za mchakato wa mazungumzo ya maridhiano ili kuwa na Taifa lenye amani na umoja na
kuendelea kuwa mfano wa utulivu katika Afrika na Dunia kwa ujumla.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Tanzania ni
salama na tulivu na ipo tayari kuendelea kupokea wageni kutoka duniani kote kwa
manufaa ya nchi zote.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akimwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa njia ya mtandao, akiwa
mkoani Dodoma.
Amesema dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni
kuhakikisha kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amani kuendelezwa.

0 Maoni