📍Ikulu, Zanzibar | 08 Novemba 2025
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Marais Wastaafu wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Mohammed Ali Shein wa Awamu ya Saba na Mhe. Amani Abeid Karume wa Awamu ya Sita, Ikulu Zanzibar.
Marais hao
wastaafu wamemtembelea Rais Dkt. Mwinyi kwa lengo la kumpongeza kwa ushindi wa
kishindo alioupata, pamoja na kupongeza hali ya amani na utulivu iliyoshuhudiwa
wakati wa Uchaguzi Mkuu.

0 Maoni