Rais Samia awasamehe waliofuata mkumbo ghasia za Oktoba 29

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevielekeza vyombo vya sheria hasa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuona uwezekano kuwafutia mashtaka vijana waliohusika kwa kufuata mkumbo katika vurugu za uchaguzi mkuu Oktoba 29, mwaka huu.

Rais Dkt. Samia ametoa msamaha huo leo Jijini Dodoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kusema kuwa kuna wakati vijana hufuata mkumbo wa uhalifu kwa ushabiki na kuna vijana wengi waliokamatwa hawakujua wanachofanya ni uhaini.

Rais Dkt. Samia amemuelekeza Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia kwa wale vijana ambao wamefuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu awafutie makosa yao.

Aidha, Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa vijana wa Tanzania, kwa kuwaeleza kuwa nchi hii imejengwa kwa amani na utulivu wa kisiasa, na kuongeza kuwa endapo wazazi wao wangeshawishika kama walivyofanya wao nchi isingekuwa na neema na maendeleo wanayoyaona.

Chapisha Maoni

0 Maoni