Mchekeshaji MC Pilipili afariki dunia akiwa safarini

 

Tanzania imepata pigo kubwa katika tasnia ya burudani kufuatia taarifa za kifo cha mchekeshaji na mshereheshaji maarufu, Emmanuel Mathias almaarufu kama MC Pilipili, kuthibitishwa kutokea leo Novemba 16, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, MC Pilipili alikuwa safarini kuelekea jijini Dodoma kwa ajili ya kazi ya ushereheshaji aliyopaswa kuifanya jioni ya leo. Hata hivyo, akiwa safarini alifariki dunia ghafla kabla ya kutimiza majukumu yake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Ernest Ibenzi na kueleza kuwa MC Pilipili afikishwa hapo akiwa tayari amefariki dunia.

Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi rasmi na familia pamoja madaktari, huku mashabiki. Wasanii wenzake na watu wa karibu wakiendelea kutoa salamu za rambirambi mitandaoni.



Chapisha Maoni

0 Maoni