Jeshi la Polisi mkoani Tarime/Rorya limemkamata mwanaume mwenye uraia pacha wa Marekani na Kenya, Charles Onkuri Ongeta (30), ambaye pia ni mwanajeshi wa Jeshi la Marekani mwenye cheo cha Sajenti, akiwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS M68.
Tukio hilo lilitokea Novemba 16, 2025 imesema Ongeta alikamatwa
mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari, wakati askari wa ulinzi wa mipaka
walipomsimamisha mtuhumiwa huyo aliyekuwa akiingia nchini akitokea upande wa
Kenya kwa kutumia gari lenye namba KDP 502 Y, aina ya Toyota Land Cruiser.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, silaha
alizokutwa nazo haziruhusiwi kuingizwa nchini hata kama angekuwa ameomba
kibali, kwani sheria za umiliki wa silaha nchini hazitumii vibali kwa vifaa vya
aina hiyo.
Jeshi la polisi limesema linaendelea kukusanywa ushahidi sambamba
na kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ziweze
kuchukuliwa dhidi yake.
Jeshi la Polisi limesema uchunguzi zaidi unaendelea kubaini lengo la mtuhumiwa kuingia nchini akiwa na mabomu hayo, huku akiendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.


0 Maoni